Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 08:37

Korea Kaskazini yafanya majaribio mengine ya makombora


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akiwa na makamanda wa jeshi lake.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akiwa na makamanda wa jeshi lake.

Korea Kaskazini ilifyatua makombora mengine Jumatano, jeshi la Korea Kusini limeripoti na kuongeza kuwa juhudi hizo za kushangaza za Pyongyang zimeongeza wasiwasi wa kijeshi Kaskazini mashariki mwa Asia.

Makombora ya masafa mafupi yalifyatuliwa kutoka eneo la Sukchon, kaskazini mwa mji mkuu Pyongyang, kwa mujibu wa mnadhimu wa jeshi la Korea Kusini.

Kikosi cha doria cha mwambao cha Japan kimesema makombora yalionekana hewani kwa chini ya dakika tano kabla ya kutua katika bahari mashariki mwa mwambao wa Korea.

Wiki iliyopita Korea Kaskazini ilifyatua makombora 34 na kusababisha kutolewa kwa tahadhari na zile za watu kujificha nchini Korea Kusini na Japan.

Mabaki ya makombora kutoka kwa moja ya kombora yalitua katika bahari ya Korea Kusini, na baadaye yalitolea na kikosi cha maji cha Korea Kusini.

XS
SM
MD
LG