Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 07:51

Korea kaskazini imefyatua makombora 23, imeonya Marekani na Korea kusini


Makombora ya Korea kaskazini yakifyatuliwa kutoka sehemu ambayo haikutajwa na serikali ya nchi hiyo.
Makombora ya Korea kaskazini yakifyatuliwa kutoka sehemu ambayo haikutajwa na serikali ya nchi hiyo.

Korea kaskazini imefyatua makombora 23 kuelekea baharini, likiwemo kombora moja ambalo limeanguka kilomita 60 kutoka pwani ya Korea kusini.

Rais wa Korea kusini Yoon Suk-yeol ametaja hatua ya Korea kaskazini kufyatua makombora hayo kuwa tendo la kuingilia mipaka yake.

Hii ni mara ya kwanza makombora ya Korea kaskazini yameanguka katika maji ya Korea kusini tangu Peninsula ya Korea ilipogawanyika mwaka 1945, n ani idadi kubwa ya makombora kuwahi kufyatuliwa na Korea kaskazini kwa siku moja.

Korea kusini imetoa onyo na kuvurumisha makombora matatu angani kama ishara ya kujibu hatua hiyo ya Jirani wake.

Mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa wa Korea kusini Kim Sung-han, amesema kwamba rais Yoon Suk-yeol amekemea kabisa hatua hiyo ya Korea kaskazini na kuitaja kuwa uchokozi, akitaka hatua za haraka kuchukuliwa kuiadhibu Korea kaskazini.

"Msimamo wetu unajulikana. Kwanza kabisa, serikali inashutumu Korea kaskazini kwa kuvunja kanuni za umoja wa mataifa kuhusu amani na makubaliano ya kijeshi nambari 9.19 kwa kutekeleza uchokozi wakati wa maombolezi. La pili ni kwamba uchochezi wowote wa korea kaskazini unaotishia raia wetu haukubaliki na serikali itafanya kila iwezalo kujibu kwa haraka na kwa nguvu zote."

Rais Yoon Suk-yeol ameongoza kikao cha usalama baada ya Korea kaskazini kuvurumisha makombora hayo.

Korea kaskazini imefyatua makombora hayo saa chache baada ya kutishia kutumia silaha za nyuklia katika kile imetaja kama kufanya Marekani na Korea kusini kulipia gharama ghali kuwahi kutokea katika historia.

Korea kaskazini imekasirishwa na mazoezi ya kijeshi yanayoendelea kati ya Marekani na Korea kusini, ikiamini kwamba ni matayarisho ya kuivamia kijeshi.

XS
SM
MD
LG