Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 00:06

Kongo yatoa ilani nyingine kwa waasi wa FDLR


Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imetoa ilani nyingine ya miezi sita kwa waasi wa Rwanda wa FDLR kuweka chini silaha kwa hiyari yao wenyewe.

Hatua hiyo inafuatia mkutano wa pamoja baina ya mawaziri wa ulinzi na mambo ya nje wa nchi wanachama wa kongamano la nchi za maziwa makuu pamoja na jumuiya ya SADC.

Kwenye mkutano na wandishi habari mjini Kinshasa msemaji wa serikali Lambert Mende amesema kwamba hatua ya kuwepo na ilani mpya kwa waasi hao inalenga kuepusha maafa ya raia wa kawaida. Hata hivyo amesema kwamba jeshi litaingilia kati ikiwa waasi hao wa FDLR watakaidi kuweka chini silaha kwa hiyari yao wenyewe kama walivyotangaza. “Kunasalia wapiganaji 1,300 ama 1,500 na hivi sasa zaidi ya 200 wametua chini silaha kwa hiyari yao wanafika zaidi ya asilimia 10, ijapokuwa bado ni wachache lakini tuko katika njia nzuri kwa hiyo nilazima tuipe bahati taratibu hii ya kujisalimisha kwa waasi hao. Bila kusahahu kwamba Rais Kabila na serikali yake wanataka FDLR wote waondoke kwenye ardhi ya Kongo”.

Ilani ya miezi sita kwa waasi hao ili watuwe chini silaha ilijadiliwa na kuridhiwa na mawaziri wa ulinzi na wale wa mambo ya nje wa nchi 11 wanachama wa kongamano la nchi za maziwa makuu ICGLR na wale wa jumuiya ya SADC kwenye mkutano wa pamoja uliomalizika mjini Luanda Angola. Lambert Mende ameeleza kwamba Kongo kwa kipindi cha miaka mingi sasa imeonyesha nia nzuri ya kuwasaka waasi hao wa FDLR. Tayari waasi 11,000 wamerejeshwa kwao Rwanda katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, alisema Lambert Mende msemaji wa serikali ya Kongo.

Lambert Mende
Lambert Mende

Wakati huo huo, serikali ya Kongo imelaani mapigano yaliyotokea mwezi Juni baina ya jeshi la Kongo na lile la Rwanda kwenye eneo la mpakani. Lambert Mende amesema kwamba mapigano hayo ni hatua ya uchokozi kutoka jirani zao wao Rwanda. Alisema serikali ya Kongo imetoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa ilikuchangia kufanikisha mkataba wa amani wa Addis-Ababa baina ya nchi wanachama wa kanda ya maziwa makuu.

Kwenye mkutano huo na wandishi wa habari bwana Mende alitoa pia msimamo wa serikali ya Kongo kuhusu ujumbe wa maaskofu wa kanisa katoliki ambao waliomba katiba isirekebishwe ili kumruhusu rais wa sasa kuwania muhula wa tatu.

Mende amesema msimammo huo wa maaskofu unawapotosha raia wa kongo kwa sababu hakuna taasisi hata moja inayopanga kubadili katiba. Mende amesema kwamba Rais Kabila ataheshimu katiba ya nchi. Aliwaomba maaskofu wa kanisa kutoegemea upande wowote na kutoingilia kati masuala ya kisiasa.

XS
SM
MD
LG