Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 04:29

Kombe la Dunia laleta utamaduni wa kimataifa Moscow


Pambano la Kundi F- Ujerumani dhidi ya Mexico. Washabiki wa Mexico wakisheherekea katika mnara wa Uhuru wa Angel, Mexico.
Pambano la Kundi F- Ujerumani dhidi ya Mexico. Washabiki wa Mexico wakisheherekea katika mnara wa Uhuru wa Angel, Mexico.

Wakati mashindano ya Kombe la Dunia yakiwa yamepamba moto, washabiki kutoka pande mbalimbali za dunia wanaendelea kuwasili nchini Russia, wengi wakiwa wanazuru nchi hiyo kwa mara ya kwanza, baada ya safari ndefu kutoka Amerika Kusini, Afrika na Asia.

Idadi kubwa ya wananchi wa Russia wanasema mashabiki hao tayari wameibadilisha miji mingi ya nchi yao.

Moscow imekuwa ni mkusanyiko wa kimataifa katika shamrashamra hizo za kombe la dunia.

Mitaa mbalimbali huko Kremlin, ambayo imewekewa ulinzi mkali na ambapo theluji huendelea kuwepo kwa muda mrefu wa mwaka, imebadilika na kuwa na vivutio vya Kilatini na midundo ya Kiafrika.

“Kila kitu ni kipya kwetu, ni utamaduni mpya, lugha mpya, na vigumu sana kufanya mawasiliano. Lakini tunashauku kubwa sana,” amesema mshabiki wa Colombia, Catarina Tejada.

Salah ambaye ni mshabiki wa Misri anasema, “Watu ni wakarimu sana, na mandhari ni nzuri sana.”

Mshabiki wa Mexico Jorge anasema, “ Sisi sote tumeungana, Wamarekani, Wazungu, Waasia. Kila mtu yuko pamoja.”

Wenyeji hawajawahi kuona kitu kama hiki.

Kila moja ni rafiki kwa mwengine. Hii ni hali ya watu kusheherekea, ni tukio lisilokuwa la kawaida, ni poa sana kuliko hata sherehe za mwaka mpya!”

Baadhi ya mashabiki hao wamesafiri kuja hapa pamoja na kuwa nchi zao zilikuwa hazijafanikiwa kuingia katika michuano hiyo, kama vile kijana wa miaka 12 Abdul Jabar kutoka Sudan.

Abdul Jabar, mshabiki kutoka Sudan : Mambo! Tuko hapa Moscow, hali ya hewa ni nzuri!?

Wananchi wa Nigeria wanaoishi Russia wametayarisha tafrija ya kuwakaribisha washabiki wanaotokea nchini kwao.

Ennie Charles, mshabiki kutoka Nigeria anasema :”Tutashinda kombe hili, ninamatumaini!”

Anthony Abugu, Mwanachi wa Nigeria anaeishi Moscow anasema :” Tunasheherekea kikamilifu. Tunataka tupate uzoefu inamaanisha nini kuwaleta wananchi wote wa Nigeria waliopo hapa pamoja. Wanapenda kusakata dansi.”

Baada ya kusheherekea kuna utamaduni kidogo unajitokeza. Vituo vya treni vya Moscow hivi sasa vimepambwa kwa rangi za timu mbalimbali wakati wageni wakitembelea mitaa mbalimbali wakiwa wanaendelea kujionea vivutio mbalimbali.

Russia inashauku ya kuonyesha vivutio vyake vya utamaduni, ikiwemo sanaa zilizojipanga katika jumba la maonyesho la Peterburg hadi maeneo yaliyokuwa hayajatambulika sana yenye urithi wa utamaduni wa Kiislam katika mji wa Kazan.

Pia kuna maelfu ya wanaojitolea kusaidia wageni, wakiwemo wale wanaozungumza lugha za kigeni wakiwa wakereketwa wa kuhakikisha michuano hiyo inafana.

XS
SM
MD
LG