Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 27, 2022 Local time: 18:13

Kombe la Dunia lafunguliwa rasmi Russia


Mashabiki wakijipiga picha nje ya Uwanja wa mpira wa Luzhniki, Moscow, Russia, Juni 14, 2018, siku ya ufunguzi wa Kombe la Dunia 2018.

Russia ambaye ni mwenyeji wa Kombe la Dunia, kandanda ya 21 inakutana na Saudi Arabia katika mechi ya ufunguzi wa dimba hilo Alhamisi.

Wachambuzi wa michezo wanasema kuwa itakuwa pigo kubwa kwa Russia endapo itashindwa na Saudi Arabia, timu ambayo inachukuwa nafasi ya 66 ulimwenguni katika viwango vya FIFA, kwa kuwa Russia itakuwa na kibarua kigumu katika mechi yake ya pili na Misri hapo Juni 19.

Kwa mujibu wa ratiba katika mechi ya tatu, Russia itakutana na Uruguay tarehe 25 Juni.

Pia moja ambalo limekuwa likizungumziwa sana ni kile kinachoelezwa kuwa Timu ya taifa hiyo inamtegemea sana golikipa wake Igor Akinfeev.

Kadhalika Rais Vladimir Putin anahudhuria sherehe za ufunguzi katika uwanja wa mpira wa Luzhniki, Moscow wenye viti 80,000.

Russia inatumia Dola za Marekani bilioni 13 kwenda na tukio hilo la Kombe la Dunia ambapo mechi zitachezwa katika miji mikuu 11.

Makundi yatacheza mpaka Juni 28 na wale watakao shindwa wataaga mashindano kuanzi Juni 30. Mshindi wa Kombe la Dunia atatangazwa Julai 15.

Brazil, France, Spain, Argentina na mtetezi wa Kombe hilo Ujerumani 2014 ni kati ya timu zinatabiriwa na wengi kushinda mashindano yenye timu 32.

Televisheni zitaonyesha mchezo huo ambao utawafikia watazamaji wengi duniani wakati pia mashabiki watakuwa wanaangalia mchezo huo Russia.

Shirikisho la Mpira wa Miguu FIFA imesema wakati wa michuano ya Kombe la Dunia 2014 takriban watu bilioni 3 walitazama angalau sehemu ya mchezo huo, na watu bilioni 1 walijiunga kuangalia mechi ya fainali iliyochezwa kati ya Ujerumani na Argentina.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG