Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 19:46

Kocha wa Black Stars anaamini timu yake itafanya vyema


Timu ya taifa ya Ghana -BlackStars Septemba 27, 2022 kabla ya mechi yao ya kirafiki na Nicaragua. REUTERS.

Kocha wa timu ya taifa ya Ghana-Black Stars  Otto Addo alikiri hatari ya kujumuisha wachezaji kadhaa wapya kwenye kikosi chake  kabla ya michuano ya Kombe la Dunia huko Qatar baadaye mwezi ujao , lakini haamini kuwa itakuwa na athari ya kuiyumbisha timu yake.

Kocha Addo, ambaye alichukua usukani Februari baada ya kampeni mbaya ya Ghana katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, na itakumbukwa hivi karibuni aliwachezesha mechi ya kwanza wachezaji Inaki Williams, Tariq Lamptey na Mohammed Salisu katika mchezo wao wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Brazil na kufungwa 3-0.

Williams mwenye umri wa miaka 28 alishinda mechi moja kwa Uhispania mwaka 2016 na Lamptey miaka 21, alicheza mara kwa mara katika timu za vijana za England kabla ya kuamua kubadili uraia.

Addo mzaliwa wa Ujerumani, ambaye aliichezea Ghana katika Kombe la Dunia la mwaka 2006, pia amewaita Ransford-Yeboah Konigsdorffer na Stephan Ambrosius, wote hao waliichezea Ujerumani chini ya umri wa miaka 21.

Daima ni hatari kupata wachezaji wapya, haswa ikiwa wachezaji waliokuwepo hapo awali watapata kitu kizuri sana, "alisema Addo, ambaye alisimamia ushindi wa mechi ya mchujo wa Kombe la Dunia dhidi ya Nigeria mwezi Machi.

Kuna kundi lenye nguvu ambalo sitaki kulivunja, lakini nadhani kutokana na nilichokiona walikaribishwa vyema.

"Walifanya vizuri kwenye mazoezi na kuelewana na hawakuwa kama wageni. Kabla wengine walijuana kutokana na kucheza ligi moja na kila kitu kiko sawa."

Addo anaamini kuwaongeza wazaliwa wa Ulaya kwenye timu kutaongeza ushindani wa nafasi na kuifaidisha Black Stars.

"Ni hali nzuri. Tuna presha kutoka kwenye benchi kwa sababu kuna watu wapya ambao wako imara sana Ulaya, na tuna wachezaji uwanjani ambao wanapaswa kujidhihirisha," alisema.

Addo alikiri kuwa "hafurahishwi sana" na aina ya ulinzi wa timu yake kwenye mipira ya kurusha , kona na free kick lakini alisisitiza kupoteza dhidi ya Brazil kumetoa fursa muhimu ya kujifunza kabla ya kuelekea Qatar.

'Timu ilikuwa mbaya'

Brazil, timu ya hali ya juu duniani , iliisambaratisha Ghana katika kipindi cha kwanza kwenye uwanja wa Le Havre, huku Richarlison akipachika mabao mawili baada ya Marquinhos kupata bao la kwanza kwa kichwa.

Bao la pili la Richarlison lilitokana na mkwaju wa Neymar, huku fowadi huyo wa Tottenham Hotspur akifunga kwa kichwa kwenye eneo la karibu na lango.

Kwa ujumla, timu ilikuwa mbaya, ukipoteza 3-0 wewe ni timu mbovu," Addo alisema baada ya Ghana kupokea kichapo cha tano katika mechi nyingi dhidi ya Brazil.

"Nilisikitishwa sana, haswa na mipira ya ya kurusha , kona na free kick walikuwa na nafasi nyingi. Tulikuwa na bahati katika baadhi ya hali ambazo hawakutufunga."

Lakini alikasirishwa na pendekezo kwamba mabingwa hao wa mara nne wa Afrika hawakuwa tayari kushiriki Kombe la Dunia.

"Ukiona ni mara ngapi (Brazil) wamefunga mabao matatu au manne, basi hakuna aliye tayari," alisema Addo.

"Siyo kama tulikuwa tunacheza dhidi ya wavulana wadogo. Hawa ni wazuri sana."

Katika Kombe la Dunia la mwaka 2018 nchini Russia hakuna timu ya Kiafrika iliyofuzu kwa awamu ya mtoano kwa mara ya kwanza baada ya miaka 36.

Ghana, ambayo ilikosa mkwaju wa penalti ya Asamoah Gyan mbali na kukosa kuingia hatua ya nusu fainali mwaka 2010, ina mchezo mmoja wa mwisho wa marudiano dhidi ya Nicaragua kabla ya Addo kukamilisha mipango yake ya Kombe la Dunia.

Tulipoteza 3-0 kwa hivyo kila mtu anafikiria hii ni timu dhaifu. Labda hii ni faida kwetu," alisema.

"Kila kitu kinaleta kitu kizuri ikiwa utajifunza kutoka kwake. Natumai kwamba nilijifunza. Labda itabidi nifanye vitu vingine tofauti. Ikiwa kila mtu anafikiria hivyo basi tutafanya vizuri zaidi. Sijali hata kidogo."

Nilifanya makosa, nitajifunza kutoka kwao natumai kuimarika," aliongeza.

"Kipindi cha pili kilionyesha tunaweza kushindana nao."

Ghana watacheza na Ureno katika mechi yao ya ufunguzi kwenye Kombe la Dunia Novemba 24. Pia wamepangwa pamoja na Uruguay na Korea Kusini katika Kundi H.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG