Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 14, 2025 Local time: 09:26

Kocha na mlinda lango wa timu ya soka ya Algeria wafariki kwenye ajali ya basi


Picha ya maktaba ya basi lililopata ajali.
Picha ya maktaba ya basi lililopata ajali.

Shirikisho la soka la Algeria limesema Alhamisi kwamba mlinda mlango na kocha msaidizi wa  timu maarufu ya soka nchini humo wamefariki katika  ajali ya basi, tukio ambalo limepelekea kusitishwa kwa mechi zote za  mwishoni mwa wiki.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, wachezaji wengine 10 kutoka kwenye timu ya MC El Bayadh, pia wamejeruhiwa kwenye ajali hiyo, iliyotokea wakati wakisafiri kuelekea mji wa kaskazini wa Tizi Ouzou, kwa mechi yao ya wikiendi dhidi ya timu ya JS Kabylie, taarifa zimesema.

Shirikisho hilo limesema basi hilo lilipata ajali karibu na mji wa Tiaret uliopo takriban kilomita 150 kutoka kwenye pwani ya Mediterranean, bila kutoa maelezo zaidi.

Forum

XS
SM
MD
LG