Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 00:55

Kizuizi kati ya Kosovo na Serbia chaondolewa mpakani


Kosovo imefungua mpaka wake na Serbia baada ya makubaliano kufikiwa juu ya kuviondoa.
Kosovo imefungua mpaka wake na Serbia baada ya makubaliano kufikiwa juu ya kuviondoa.

Kosovo imefungua mpaka wake na Serbia baada ya makubaliano kufikiwa juu ya kuondoa kizuizi.

Rais wa Serbia ametangaza njia nyingine zinazounganisha nchi hizo mbili kaskazii mwa Kosovo zitafunguliwa.

Rais Aleksandar Vucic amesema kwamba utawala wa Serbia utaanza kuondoa vizuizi katika mipaka yote ya kaskazini mwa Kosovo kuanzia Alhamisi.

Hatua hiyo inatarajiwa kupunguza uhasama wa wiki kadhaa ambao umetishia kutokea mapambano katika eneo la Balkans.

Vucic amesema kwamba makubaliano yalifikiwa katika kikao kilichofanyika usiku na viongozi wa Kosovo wenye asili ya Kiserbia.

Hatua hiyo inafanyika baada ya kuachiliwa kwa aliyekuwa polisi wa Kosovo mwenye asili ya kiserbia, ambaye kukamatwa kwake kulipelekea mgogoro mkubwa kati ya Serbia na Kosovo na kusababisha wasiwasi kimataifa.

Polisi wa Kosovo wameambia watu kwamba wanaweza kutumia mpaka huo kuingia Kosovo badala ya kupitia North Macedonia au nchi zingine.

Mgogoro unatokana na mashambulizi ya mwaka 1998 – 1999 ya watu waliotaja kujitenga na Kosovo, wengi wao wakiwa Albania, na kusababisha msako mkali wa maafisa wa usalama.

XS
SM
MD
LG