Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 11:06

Kituo cha polisi kenya chashambuliwa


Mashambulizi ya mabomu yalitokea pia katika nyumba za starehe na makanisa huko kenya
Mashambulizi ya mabomu yalitokea pia katika nyumba za starehe na makanisa huko kenya
Polisi huko Mombasa nchini Kenya imedhibitisha kuwa mwenzao mmoja amejeruhiwa baada ya bomu la kutengenezwa kwa petroli kutupwa katika kituo kimoja cha polisi.

Tukio hilo lilitokea jumapili usiku katika kituo kidogo cha polisi cha Kiembeni kwenye eneo la Kisauni pale watu wawili walipojifanya kukitembelea kituo hicho kwa nia ya kuandika ripoti ya polisi ndipo wakapata fursa ya kurusha bomu hilo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:37 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Afisa mkuu wa polisi mkoani humo, Aggrey Adoli amesema askari mmoja aliyekuwa kazini wakati huo alijeruhiwa na anapata matibabu katika hospitali moja mjini humo.

Msako umekuwa ukiendelea kufuatia tukio hilo huku ikisemekana washukiwa watatu wa bomu hilo pia walijeruhiwa kwa risasi na maafisa wengine wa polisi waliokuwepo kituoni hapo.

Matukio ya polisi kushambuliwa yameongezeka nchini Kenya mwaka huu kutokana na idadi ya watu wanaotajwa na vyombo vya usalama kuwa ni washirika wa makundi ya kigaidi.

Hata hivyo usalama umeimarishwa katika sehemu mbali mbali pia katika vituo vya polisi ili kuzuia wizi wa silaha.

Katika taarifa tofauti inayolenga usalama wa taifa Waziri Mkuu Raila Odinga alisema mazungumzo na viongozi wa kundi la vuguvugu la Mombasa Republican Council–MRC yatafungua nyoyo za wafuasi wao.

Waziri Mkuu alikuwa Mombasa kuongoza mkutano wa kisiasa wa chama cha ODM anasema ameshauri viongozi wa kundi hilo kukubali kuchukua kura tayari kwa uchaguzi mkuu utakaofanyika mapema mwaka ujao, pamoja na kuwarai wafuasi wao kote mkoani humo.

Wachanganuzi wa maswala ya kisiasa wanaiona hatua ya Bwana Odinga kama ushawishi wa kisiasa anapowania kiti cha urais wa Kenya katika uchaguzi mkuu ujao.

Wakati huo huo MRC inataka wafuasi wao wote waliokamatwa na kuwekwa jela waachiwe huru kutoka gerezani.
XS
SM
MD
LG