Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 08:37

Kituo cha kutibu Ebola chaporwa


Wafanyakazi wa afya wabeba maiti ya mgonjwa wa Ebola, Monrovia, Liberia Agosti 12, 2014
Wafanyakazi wa afya wabeba maiti ya mgonjwa wa Ebola, Monrovia, Liberia Agosti 12, 2014

Kundi moja la wakazi wenye silaha, wengi wao wanaume waliokuwa na virungu, walivunja jengo na kuiba vifaa kutoka kituo cha afya ambavyo huenda vimeathiriwa na virusi vya Ebola.

Waandamanaji nchini Liberia walishambulia na kupora mali kwenye kituo kimoja kilichowekewa karantini kwa wagonjwa wa Ebola katika mji mkuu wa Monrovia.

Maafisa wanasema shambulizi lilitokea Jumamosi jioni kwenye kituo kilichopo katika mji jirani wa West Point. Wanasema kundi moja la wakazi wenye silaha, wengi wao wanaume waliokuwa na virungu, walivunja jengo na kuiba vifaa kutoka kituo cha afya ambavyo huenda vimeathiriwa na virusi vya Ebola.

Shirika la habari la Ufaransa-AFP, linawakariri wafanyakazi wa afya wa Liberia wakisema kwamba wagonjwa 20 ambao wote walifanyiwa uchunguzi na kugunduliwa wana virusi vya Ebola, pengine walikimbia baada ya shambulizi au walilazimishwa kuondoka na jamaa zao.

XS
SM
MD
LG