Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 27, 2022 Local time: 01:39

Waandishi habari wahofia maisha yao Kenya


Wafanyakazi wa Al Jazeera wakiandaa habari kutoka studio za Doha, Qatar

Ripoti ya kituo cha televisheni cha Al Jazeera chenye makao makuu yake Doha huko Qatar, kuhusu ukatili na mauwaji ya kiholele yanayodaiwa kufanywa na wa polisi wa Kenya, imezusha wasi wasi miongoni mwa wanaharakati wa kutetea haki za binadam na waandishi habari nchini humo.

Wasi wasi huo unatokana na kwamba, mwandishi habari mashuhuri wa Kenya Mohamed Ali wa makala ya "Jicho Pevu" katika kituo cha televisheni KTN anaesemekana aliisaidia Al-Jazera kutayarisha makala hayo amelazimika kwenda mafichoni.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:00 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Ritpoti hiyo ya televisheni inaeleza kwamba baadhi ya maafisa wa polisi ambao hawakutaka kutajwa wameeleza kwamba kuna kitengo maalum ndani ya kikosi cha polisi ambacho kinaanda mauaji hayo ta kiholela dhidi ya viongozi wa kiislam wenye msimamo mkali.

Msemaji wa Polisi wa Kenya Masud Mwinyi anasema polisi wa Kenya hawajakiri kuwepo na mauwaji ya aina hiyo yanayofanywa na kikosi chake.

Na maafisa wa serikali wanasema watu walioandaa ripoti hiyo ya Al Jazeera hawakutilia maanani maisha ya Wakenya wengi wasio na hatia ambao waliuwawa na magaidi nchini humo.

Mwenyekiti wa wa kunri la kutetea haki za Binadam Haki Afrika Hussein Khalid, ameiambia Sauti ya Amerika kwamba wamemsaidia Ali kwenda mafichoni na hali hiyo inatishia haki msingi wa waandishi habari nchini humo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:05:56 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

XS
SM
MD
LG