Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 21:56

Kipchoge avunja rekodi nyingine ya dunia


Mwanariadha wa Kenya Eliud Kipchoge akisherehekea jukwaani baada ya kushinda Berlin Marathon na kuvunja Rekodi ya Dunia REUTERS/Fabrizio Bensch.
Mwanariadha wa Kenya Eliud Kipchoge akisherehekea jukwaani baada ya kushinda Berlin Marathon na kuvunja Rekodi ya Dunia REUTERS/Fabrizio Bensch.

Bingwa mara mbili wa Olimpiki Eliud Kipchoge kutoka Kenya kwa mara nyingine tena amevunja rekodi yake ya dunia katika mbio za Marathon za Berlin Ujueumani siku ya Jumapili.

Nyota huyo wa Kenya alitumia saa 2, dakika 1, sekunde 9 na kupunguza sekunde 30 kutoka kwa muda wake wa awali wa saa 2:01:39 katika njia ile ile alioweka rekodi yake ya 2018.

"Miguu yangu na mwili wangu bado unajihisi kijana," Kipchoge mwenye umri wa miaka 37 alisema. "Lakini jambo muhimu zaidi ni akili yangu, na hiyo pia inahisi mpya na mchanga. Nina furaha sana kuvunja rekodi ya dunia.”

Kipchoge, amejivunia rekodi zake ambazo hakuna mtu yeyote aliyeweza kuweka kwenye mbio za Marathon, kwa kuweza kushinda mbio 15 kati ya 17 za kimataifa, ikiwa ni sio tu medali mbili za dhahabu za mbio za Olimpiki bali ushindi katika michuano kumi tofauti ya dunia.

Mwanariadha wa Ethiopia, Tigist Assefa alishinda bila kutarajia katika mbio za wanawake akivunja rekodi yake binafsi kwa kwenda mbio akitumia muda wa saa 2:15:37 , ikiwa ni dakika 18 mbio zaidi kuliko alivyowahi kukimbia hapo awali. Ilikuwa mbio za tatu kwenda na kasi kubwa kwa wanawake.

"Sikuwaogopa wapinzani wangu, ingawa walikuwa na nyakati za haraka kuliko mimi," Assefa mwenye umri wa miaka 26 alisema.

Rosemary Wanjiru wa Kenya alikuwa wa pili katika mbio yake ya kwanza ya Marathon akitumia muda wa saa 2:18:00, ikiwa ni mara ya pili kwa mtu kuingia kwenye mbio hizo kwa mara ya kwanza na kwenda kwa kasi kama hizo mbele kidogo ya ile iliyowekwa na mwanariadha wa Ethiopia Tigist Abayechew alipotumia saa 2:18:03.

XS
SM
MD
LG