Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 27, 2025 Local time: 04:14

Kiongozi wa zamani wa Ujerumani afariki dunia


Hans Modrow, ambaye alihudumu kama kiongozi wa mwisho wa kikomunisti wa Ujerumani Mashariki wakati wa kipindi kilichokuwa na misukosuko ambacho kilimaliza  uchaguzi wa kwanza na pekee huru, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95. 

Modrow amefariki dunia mapema Jumamosi, kundi la wabunge wa chama cha mrengo wa kushoto walitweet.

Modrom, mkomunisti aliyekuwa na mawazo ya kimageuzi, alichukua madaraka ya Ujerumani Mashariki muda mfupi baada ya kuvunjwa kwa ukuta wa Berlin, na baadaye kuyaalika majeshi ya upinzani kuingia katika serikai, lakini hakuweza kupunguza kasi ya harakati kwa muugano wa Ujerumani.

Wakati wa kipindi cha miaka 16 kama mkuu wa chama cha kikomunisti huko Dresden, kuanzia mwaka 1973, Modrow alijijengea sifa ya kukabiliana na wanasiasa mashuhuri.

Alikataa vitu alivyopewa na chama na kusisitiza kukaa nyumba ya nyumba ya kawaida.

XS
SM
MD
LG