Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 00:31
VOA Direct Packages

Kiongozi wa upinzani wa Belarus apewa kifungo cha miaka 15 jela kwa tuhuma za kupanga mapinduzi


Kiongozi wa upinzani wa Belarus Sviatlana Tsikhanouskaya aliyeko uhamishoni Poland.
Kiongozi wa upinzani wa Belarus Sviatlana Tsikhanouskaya aliyeko uhamishoni Poland.

Kiongozi wa upinzani wa Belarus Sviatlana Tsikhanouskaya, aliyeko uhamishoni, Jumatatu amepewa kifungo cha miaka 15 jela, licha ya kutokuwepo nchini, baada ya kupatikana na hatia ya jaribio la mapinduzi.

Uamuzi huo yeye ameutaja kuwa adhabu ya kujaribu kukuza demokrasia ya Belarus. Tsikhanouskaya mwenye umri wa miaka 40 na ambaye aliwahi kuwa mwalimu wa kiingereza alikimbilia kwenye nchi jirani ya Lithuania mwaka 2020, baada ya kugombea uchaguzi wa rais dhidi ya kiongozi wa sasa Alexander Lukashenko, ambao matokeo yake yalionyesha kuwa Lukashenko alishinda kwa asilimia kubwa.

Hata hivyo Tsikhanouskaya pamoja na upinzani walipinga matokeo hayo wakidai kuwa uchaguzi uliibwa. Madai hayo yalikanushwa vikali na Lukashenko ambaye ametawala Belarus kimabavu kwa karibu miongo mitatu. Hali hiyo ilipelekea maandamano makubwa ya kitaifa dhidi ya utawala wa Lukashenko ambaye ni rafiki wa karibu wa rais wa Russia Vladimir Putin, wakati maafisa wa usalama wakikamata wapinzani na kulazimisha baadhi yao kutoroka nchini.

XS
SM
MD
LG