Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 15, 2024 Local time: 02:28

Kiongozi wa upinzani Ufaransa akemea kundi la M23


Kiongozi wa upinzani wa  Ufaransa mwenye msimamo mkali wa mrengo wa kushoto, Jean-Luc Melenchon, Alhamisi, amekemea “kujipanua kwa Rwanda,” mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wakati mapigano yakiendelea baina ya waasi na makundi yanayo unga mkono serekali.

Kiongozi huyo baada ya kukutana na rais wa DRC, Felix Tshisekedi, amesema kwamba anataka kuwahakikishia kwamba anawaunga mkono watu wa DRC, wakati wanapokabiliana na changamoto ambazo zimeletwa nchini mwao.

Ulikuwa wasaa wa kushutumu matendo yanayo vuruga maisha ya kidemokrasia, toka kuanza kwa shughuli za kijeshi zikifanyika wakati DRC inaandaa uchaguzi wa rais Desemba 20, ambapo rais Tshisekedi ni mgombea.

Wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa, Kinshasa, Paris, pamoja na Washington, zimeshutumu Rwanda, kusaidia harakati za kundi la waasi wa Kitutsi la M23, ambalo limeshikilia udhibiti wa maeneo kadhaa mashariki mwa DRC toka mwaka 2021.

Kigali daima imekanusha kuhusika na kundi hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG