Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 12, 2025 Local time: 08:59

Kiongozi wa upinzani Senegal afikishwa mahakamani kwa tuhuma za ubakaji


Mkusanyiko wa wafuasi wa upinzani walipokuwa wakicheza muziki kwenye mkutano wa upinzani nchini Senegal wakati wa uchaguzi.
Mkusanyiko wa wafuasi wa upinzani walipokuwa wakicheza muziki kwenye mkutano wa upinzani nchini Senegal wakati wa uchaguzi.

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Senegal alifikishwa katika mahakama moja ya Dakar kutokana na tuhuma za ubakaji kwa mara ya kwanza siku ya Alhamisi, huku wakili wake akiitaja kesi hiyo kuwa ni njama ya taifa ambayo inapaswa kutupiliwa mbali.

Ousmane Sonko, mwenye umri wa miaka 48, alishtakiwa mwaka jana kwa kumbaka mfanyakazi wa saluni ambapo alikuwa akifanyiwa masaji.

Kukamatwa kwake na kufunguliwa mashtaka mnamo mwezi Machi 2021 kulisababisha ghasia mbaya za siku kadhaa nchini Senegal, taifa ambalo kwa kawaida linatazamwa kama mwanga wa utulivu katika eneo la Afrika Magharibi lenye hali tete ya kisiasa.

Sonko anadai Rais wa Senegal Macky Sall anajaribu kutega mtego kwa ajili yake na wafuasi wake na Jumatano aliomba utulivu, akiwataka kutokukusanyika nje ya mahakama.

Kesi ya Alhamisi katika mji mkuu wa Senegal ilidumu kwa saa tatu. Usalama mkubwa uliwekwa katika jiji lote, haswa karibu na nyumba ya Sonko na jengo la mahakama.

Mamlaka imekanusha matumizi yeyote mabaya ya taasisi za serikali katika kesi dhidi ya Sonko, ambaye aliibuka wa katika nafasi ya tatu katika uchaguzi uliopita wa urais mwaka wa 2019 na anapanga kugombea tena mwaka 2024.

XS
SM
MD
LG