Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 20:20

Kiongozi wa upinzani Mali Soumaila Cisse afariki kutokana na Corona


Soumaila Cisse (katikati)
Soumaila Cisse (katikati)

Kiongozi wa upinzani nchini Mali Soumaila Cisse, aliyekuwa ametekwa nyara na makundi ya wapiganaji kwa muda wa miezi sita, amefariki dunia.

Kulingana na familia yake, Cisse amefariki akiwa nchini Ufaransa baada ya kuambukizwa virusi vya Corona.

Alikuwa na umri wa miaka 71.

Alikuwa amepelekwa Ufaransa kwa matibabu maalum baada ya kugundulika kaambukizwa virusi vya Corona.

Cisse alitekwa nyara mwezi Machi tarehe 25 na watu wasiojulikana, alipokuwa katika kampeni wakati wa uchaguzi wa wabunge, katika eneo la Timbukutu, kaskazini magharibi mwa Mali.

Aliachiliwa huru mwezi Oktoba, miezi sita baada ya kuzuiliwa na wapiganaji.

Aliachiliwa pamoja na raia wa Ufaransa Sophie Petronin na watu wengine wawili, raia wa Italia.

Wote waliachiliwa baada ya serikali ya Mali kukubali kuwaachilia huru wapiganaji 200, kufuatia ombi la makundi ya wapiganaji.

Cisse alishindwa katika uchaguzi wa rais nchini Mali, mara tatu.

Mwaka 2013 na 2018, alishindwa na Ibrahim Boubacar Keita, ambaye alipinduliwa na jeshi Agosti tarehe 18 mwaka huu.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG