Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 06:33

Kiongozi wa upinzani Malawi afikishwa mahakamani kwa njama ya kumuua Rais.


Ramani ya Malawi na nchi zilizo karibu nazo.
Ramani ya Malawi na nchi zilizo karibu nazo.

Polisi nchini Malawi walimkamata Kaliati, katibu mkuu wa chama cha upinzani cha UTM wiki iliyopita kwa kupanga uhalifu.

Kiongozi wa upinzani nchini Malawi, Patricia Kaliati alifikishwa katika mahakama ya Lilongwe leo Jumatatu, ambapo alishtakiwa rasmi kwa kupanga njama za kumuua rais Lazarus Chakwera.

Polisi nchini Malawi walimkamata Kaliati, katibu mkuu wa chama cha upinzani cha United Transformation Movement (UTM), Alhamisi iliyopita kwa kupanga uhalifu. Kaliati, mbunge tangu mwaka 1999 ambaye ameshikilia nyadhifa kadhaa za uwaziri anaongoza UTM ya makamu wa rais wa zamani Saulos Chilima, aliyefariki katika ajali ya ndege mwezi Juni.

Kufuatia kifo chake, chama hicho kilijitoa katika muungano wa vyama tawala ambao uliungana ili kuwezesha muungano wa Chakwera kushinda uchaguzi wa 2020. Wakili wa Kaliati Khwima Mchizi alisema, “Mteja wangu ameamua kukaa kimya kwa kuwa anaamini hana hatia. Tunasubiri tu uamuzi wa dhamana wa mahakama” unaotarajiwa baadaye leo.

Wakati Kaliati mwenye miaka 57 alipokuwa akifikishwa mbele ya hakimu Roderick Michongwe, Chakwera alikuwa aliwaapisha wajumbe wa tume ya uchunguzi kuchunguza mazingira yaliyosababisha kifo cha makamu wa rais wa nchi hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG