Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 04:24

Kiongozi wa SLA-Unity, Darfur auwawa


Saleh Mohammed Jerbo Jamus, akiwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu huko, The Hague, June 17, 2010.
Saleh Mohammed Jerbo Jamus, akiwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu huko, The Hague, June 17, 2010.
Mawakili wa raia mmoja wa Sudan anayekabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa vita katika mahakama ya ICC wanasema mteja wao ameuwawa.

Timu ya utetezi ya Saleh Mohammed Jerbo Jamus kiongozi wa uasi katika mkoa wa Darfur nchini Sudan wanasema aliuwawa April 19 wakati wa shambulizi moja lililofanywa na kundi moja la upinzani la uasi.

Mawakili waliifahamisha mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC juu ya kifo cha Jerbo kwa njia ya maandishi yaliyowasilishwa wiki hii na kuwekwa hadharani Jumanne jioni. Mawakili waliialika mahakama kuthibitisha kifo hicho.

Jerbo alikuwa kiongozi wa zamani wa kundi la uasi la SLA-Unity katika mkoa wa Darfur ambalo baadaye liliungana na kundi jingine la uasi la The Justice and Equality Movement.

ICC ilimfungulia mashtaka Jerbo na kiongozi mwingine wa uasi Abdalla Banda Abakaer Nourain, kwa makosa matatu ya uhalifu wa vita kutokana na shambulizi moja la Septemba mwaka 2007 ambalo liliuwa walinda amani wa Umoja wa Afrika 12.

Jerbo alishirikiana na ICC na alifikishwa mara ya kwanza katika mahakama ya The Hague mwezi Juni mwaka 2010, muda mfupi baada ya kufunguliwa rasmi mashtaka ya uhalifu.

Mawakili wake wanasema shambulizi ambalo lilimuuwa lilifanywa na kundi la Justice and Equality Movement linaloongozwa na Gibril Ibrahim.
XS
SM
MD
LG