Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 15:00

Kiongozi wa Libya aapa kupigana mpaka mwisho.


Kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi
Kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi

Ndege za kijeshi za Nato zimepiga kwa kiasi kikubwa nchini Libya tangu kuanza kwa kampeni za majeshi ya muungano nchini humo.

Kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi ameapa kupigana mpaka mwisho wakati ndege za kijeshi za Nato zikipiga Tripoli kwa kiasi kikubwa tangu majeshi hayo ya muungano kuanza kampeni zake mwezi Machi.

Katika taarifa yake ya sauti kwenye televisheni ya taifa jumanne Bw. Gadhafi alisema watu wa Libya hawatajisalimisha na watakaa nchini mwao mpaka mwisho.

Televisheni ya taifa baadaye ilionyesha picha za kile walichokiita mkutano baina ya Moammar Gadhafi na viongozi wa kikabila .

Kiongozi huyo wa Libya alionekana siku za nyuma kwenye televisheni ya taifa mwishoni mwa mwezi uliopita.

XS
SM
MD
LG