Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 21, 2024 Local time: 06:09

Kiongozi wa kundi la Wagner, aonekana katika video akiwa Belarus na wanajeshi wake


Kiongozi wa mamluki wa Russia, Yevgeny Prigozhin
Kiongozi wa mamluki wa Russia, Yevgeny Prigozhin

Video iliyotolewa Jumatano inaonekana kumuonyesha mkuu wa kundi la mamluki wa Russia Yevgeny Prigozhin kwa mara ya kwanza tangu alipoongoza uasi wa muda mfupi mwezi uliopita.

Anaonekana akiwaambia wanajeshi wake kwamba watakaa kwa muda fulani Belarus kupewa mafunzo ya kijeshi kabla ya kupelekwa barani Afrika.

“Karibuni. Nafurahi kuwasalimu nyote. Karibuni kwenye ardhi ya Belarus”, video ilimuonyesha akisema.

“Tulipigana kwa heshima. Tumeitendea mengi Russia,” aliongeza.

Uasi wa Prigozhin, ambao ulikuwa tishio kubwa zaidi kwa utawala wa miaka 23 wa Rais Vladimir Putin, ulielezewa na kiongozi huyo wa mamluki kuwa ulilenga kuwaondoa viongozi wakuu wa jeshi la Russia ambao aliwashtumu kuwa wazembe.

Ukosoaji wa Prigozhin juu ya uendeshaji wa mapigano nchini Ukraine ulirudiwa katika video hiyo mpya, ambayo uhalisi wake haukuweza kuthibitishwa mara moja.

“Kinachoendelea kwenye uwanja wa mapigano leo ni aibu ambayo hatupaswi kuhusishwa nayo,” alisema, akiongeza kuwa wanajeshi wa Wagner wanaweza kurejea Ukraine katika siku zijazo.

Forum

XS
SM
MD
LG