Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 00:43

Kiongozi wa kidini Uturuki ahukumiwa miaka 8,658 jela .


Adnan Oktar

Adnan Oktar, aliongoza vipindi vya televisheni akionekana kuzungukwa na wanawake waliojipodoa sana na wakiwa wamevaa nguo ambazo hazikuwa zikiwastiri vyema, huku akionekana kuhubiri kuhusu maadili ya uumbaji na thamini za kihafidhina.

Mahakama moja ya mjini Istanbul nchini Uturuki Jumatano imemhukumu kiongozi mmoja wa kiislamu kifungo cha miaka 8,658 kwa kujihusisha na wanawake ambao hawakuwa wamejistiri vizuri aliokuwa akiwaita “paka”, chombo cha habari katika eneo hilo kimeripoti.

Adnan Oktar, aliongoza vipindi vya televisheni akionekana kuzungukwa na wanawake waliojipodoa sana na wakiwa wamevaa nguo ambazo hazikuwa zikiwastiri vyema, huku akionekana kuhubiri kuhusu maadili ya uumbaji na thamini za kihafidhina.

Mwaka jana, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 66 alihukumiwa kifungo cha miaka 1,075 jela kwa uhalifu ikiwa ni pamoja ya manyanyaso ya kingono, manyanyaso ya kingono kwa watoto wadogo, ubadhirifu na jaribio la ujasusi wa kisiasa na kijeshi.

Hata hivyo hukumu hiyo ilibadilishwa na mahakama ya juu.

Polisi wa Uturuki wakimkamata Adnan Oktar, mjini Istanbul, July 11, 2018
Polisi wa Uturuki wakimkamata Adnan Oktar, mjini Istanbul, July 11, 2018

Shirika la habari la Anadolu limeripoti kuwa, wakati wa kusikilizwa upya kesi hiyo, mahakama kuu ya uhalifu ya Istanbul, ilimhukumu Oktar kifungo cha miaka 8,658 kwa mashtaka kadhaa pamoja na manyanyaso ya kingono, na kuwanyima baadhi ya watu uhuru wao.

Mahakama pia imewahukumu watu 10 wengine kifungo kama hicho cha miaka 8,658 jela, shirika hilo la habari limeripoti.

Oktar ambaye wakosoaji wanamuona kuwa ni kiongozi wa kundi fulani la kidini, alipata umaarufu kwa vipindi vyake vilivyorushwa kupitia televisheni ya A9 kwa njia ya mtandao, amekuwa mara kwa mara akishutumiwa na viongozi wa kidini nchini Uturuki.

Katika msako mkubwa uliofanywa kwa kundi lake, alitiwa mbaroni mjini Istanbul mwaka 2018 kama sehemu ya uchunguzi wa kitengo cha uhalifu wa kifedha cha polisi mjini humo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG