Taarifa kutoka kwa kamandi hiyo, CENTCOM, imesema kwamba Usamah al Muhajir aliuwawa kwenye shambulizi la Ijumaa, Kamanda wa CENTCOM Jenerali Michael Erik Kurilla amesema kwamba , “ Tumeweka bayana kwamba tutaendelea na azma yetu ya kuishinda ISIS kote kwenye eneo hilo,” akiongeza kwamba kundi hilo limeendelea kuwa tishio siyo tu kieneo lakini pia kwenye sehemu nyinginezo. Taarifa imeongeza kusema kwamba operesheni dhidi ya ISIS kwa ushirikiano na vikosi nchini Iraq na Syria itaendelea kufanikisha kushindwa kwa kundi hilo.
Forum