Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 19:10

Taliban yateua kiongozi mkuu mpya


Wanamgambo wa Taliban nchini Afghanistan wamesema Mawlawi Haiba-Tullah Akhund-Zada ameteuliwa kuwa kiongozi mkuu wa kundi hilo, kufuatia kifo cha Mullah Akhtar Mansoor.

Katika taarifa iliyotolewa kwa lugha ya Kipashto leo Jumatano, Taliban pia imedhibitisha kwamba Mansoor aliuawa katika shambulizi la ndege ya Kimarekani isiyo na rubani au 'drone' wiki iliyopita.

Taarifa hiyo ilisema kuwa Mawlawi Haiba-Tullah Akhund-Zada ameteuliwa kuwa kiongozi mpya wa milki ya kiislamu ya Taliban, baada ya makubaliano ya pamoja ya baraza kuu, ambalo linafahamika kama Shura. Taarifa hiyo iliongeza kwamba wanachama wote wa Shura, waliapa uaminifu wao kwa kiongozi huyo mpya.

Rais wa Marekani, Barack Obama, alidhibitisha siku ya Jumatatu kwamba Mansoor aliuawa kwa sababu alikuwa kizingiti katika juhudi za kutafuta amani na Maridhiano nchini Afghanistan.

Kiongozi huyo mpya wa Taliban alikuwa ni naibu wake Mansoor, akiwa pamoja na Sira-Juddin Haqqani, ambaye ndiye kiongozi wa mtandao unaofahamika wa Haqqani.

XS
SM
MD
LG