Akikutana na makamanda wakuu wa jeshi la Iran Jumapili, Khamenei alivipongeza vikosi vya jeshi kwa mafanikio yao katika matukio ya hivi karibuni. Alikuwa akizungumzia shambulio la anga la Iran dhidi ya Israel Aprili 13.
Vikosi vya jeshi vilionyesha taswira nzuri ya uwezo na nguvu zao na taswira ya kustaajabisha ya taifa la Iran, Khamenei alisema. Pia zilithibitisha kuibuka kwa nguvu ya azma ya taifa la Iran katika ngazi ya kimataifa, aliongeza.
Forum