Hali mbaya ilitabiriwa Jumamosi katika sehemu za majimbo ya Massachusetts na Maine. Hali ya kimbunga inaweza kukumba majimbo ya Canada ya New Brunswick na Nova Scotia. Huko ndiko dhoruba hiyo inatarajiwa kuwasili baadaye mchana.
Hivi sasa kimbunga cha majira ya joto kimegeuka kuwa dharuba kali.. Hali ya dharura imetangazwa katika majimbo ya Massachusetts na Maine. Shirika la huduma za umeme limeripoti maelfu ya wateja hawana umeme kutoka Maine hadi Nova Scotia Canada.
Forum