Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 05:43

Kimbunga Freddy nchini Malawi kimesababisha vifo takribani 190


Mfano wa maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Freddy huko Blantyre nchini Malawi
Mfano wa maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Freddy huko Blantyre nchini Malawi

"Tuliwapata watu wakiwa kwenye miti, kwenye mapaa au kwenye maeneo ya juu," msemaji wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Malawi, Felix Washoni aliliambia shirika la habari la AFP. Ni changamoto kuwafikia mahala waliko, maji ni mengi na madaraja yamevunjika

Waokoaji walijitahidi Jumatano kuwafikia manusura katika mji uliokumbwa na kimbunga Freddy nchini Malawi wa Blantyre baada ya kimbunga hicho kupiga kusini mwa Afrika kwa mara ya pili na kusababisha mafuriko pamoja na maporomoko ya ardhi ambayo yamepelekea vifo vya zaidi ya watu 200.

Hali ya hewa ilitarajiwa kuimarika huku kimbunga hicho kikisambaa katika ardhi baada ya siku kadhaa za mvua kubwa lakini viwango vya mafuriko vimesalia kuwa juu katika baadhi ya maeneo yanayokwamisha juhudi za dharura. "Tuliwapata watu wakiwa kwenye miti, kwenye mapaa au kwenye maeneo ya juu," msemaji wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Malawi, Felix Washoni aliliambia shirika la habari la AFP. Ni changamoto kuwafikia mahala waliko, maji ni mengi na madaraja yamevunjika.

Kimbunga Freddy kilirudi kusini mashariki mwa Afrika mwishoni mwa wiki kwa mara ya pili katika muda wa chini ya wiki tatu huku kukiwa na vifo na uharibifu.

Serikali ya Malawi imesema watu wasiopungua 190 wameuawa huku wengine 584 wakijeruhiwa na wengine 37 hawajulikani walipo wakati mamlaka katika nchi jirani ya Msumbiji ikiripoti vifo 21 na wengine 24 kujeruhiwa.

XS
SM
MD
LG