Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 13:53
VOA Direct Packages

Kim Jong Un aongoza maadhimisho ya 75 tangu kubuniwa kwa jeshi la taifa la watu wa Korea kaskazini.


Kim Jong Un akiwa ameketi kulia pamoja na binti yake na mke wa wakati wa maadhinisho hayo.
Kim Jong Un akiwa ameketi kulia pamoja na binti yake na mke wa wakati wa maadhinisho hayo.

Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un, mke wake pamoja na binti yake Jumanne usiku wamehudhuria maadhimisho ya 75 tangu kubuniwa kwa jeshi la taifa la watu wa Korea kaskazini.

Televisheni ya kitaifa mapema Jumatano imeonyesha picha kutoka kwenye sherehe hizo, zikionyesha Kim akitoa hotuba ya kupongeza jeshi lake. Binti yake alionekana akiwa karibu naye wakati wote wa hafla hiyo. Jumatano ndiyo siku rasmi ya kuadhimisha kubuniwa kwa jeshi la kawaida la taifa hilo, tarehe ambayo ilianza kuadhimishwa tena hapo 2015.

Kwa miongo kadhaa Korea kaskazini iliadhimisha Aprili 25 kama siku ya kijeshi, ikiwa siku ambayo mwanzilishi wa taifa hilo Kim Il Sung alibuni kikosi chake cha wapiganaji ,ili kukabiliana na Japan baada ya kujinyakulia Peninsula ya Korea.

XS
SM
MD
LG