Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 21:53

Kikosi cha UN chaondoka kwenye kituo kimoja nchini Mali


Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini Mali

Kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali kimesema Jumapili kwamba kimeondoka kutoka katika kituo kimoja  kaskazini mwa nchi, kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama.

Ripoti zimeongeza kuwa wanajeshi watatu walijeruhiwa kufuatia mashambulizi saa chache baada ya ripoti ya kuondoka kutolewa. Kuondoka kwa kikosi hicho cha MINUSMA kutoka Ber kumekuja baada ya jeshi la Mali kusema Jumamosi kwamba wanajeshi 6 walikufa pamoja na wapiganaji 24 kutoka kundi la kigaidi kufuatia ghasia kwenye eneo hilo Ijumaa iliyopita.

Waasi wa zamani kutoka kabila la Tuareg wamesema kwamba jeshi pamoja na kundi la mamluki la Wagner kutoka Russia waliwashambulia wanajeshi wa MINUSMA Ijumaa, kwenye kituo cha Ber. Ujumbe wa Jumapili ulisema kwamba msafara wa MINUSMA uliokuwa ukiondoka Ber ulishambuliwa mara 2, wanajeshi watatu walijeruhiwa na kupelekwa mjini Timbuktu kwa matibabu.

Forum

XS
SM
MD
LG