Hatua hiyo imefikiwa siku moja baada ya vikosi vya akiba RSF kuweka kambi Wad Madani, ambako mashambulizi yao yamesababisha maelfu ya watu kuukimbia mji wa pili wa Sudan na kituo cha zamani cha misaada, wengi wao wakiwa tayari wameyahama makazi yao.
Kikosi cha akiba RSF kilichukua udhibiti wa Rufaa, kilomita 40 kaskazini mwa Wad Madani, mashuhuda waliiambia AFP.
Wamesema RSF ilichukua udhibiti wa makao makuu ya jeshi, kituo cha polisi, na hospitali baada ya mapigano yaliyodumu kwa saa moja katika mji huo.
Toka mapigano yaanze Aprili 15 kati ya mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na makamu wake wa zamani, kamanda wa RSF Mohamed Hamdan Daglo, mji wa Wad Madani, umekuwa kimbilio la maelfu ya watu waliokimbia makazi yao.
Forum