Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 14, 2024 Local time: 23:51

James Mattis asema uwiano wa nguvu za kijeshi kimataifa uko hatarini


Jenerali mstaafu James Mattis akiwa mbele ya kamati ya seneti ya huduma za kijeshi. Jan. 12, 2017.
Jenerali mstaafu James Mattis akiwa mbele ya kamati ya seneti ya huduma za kijeshi. Jan. 12, 2017.

Amesema yeye na rais mteule wamefanya mazungumzo juu ya umuhimu wa umoja wa majeshi ya NATO ambao ameuelezea kuwa na mafanikio makubwa “pengine milele.

Chaguo la rais mteule wa Marekani, Donald Trump ambaye ataongoza Wizara ya Ulinzi, mstaafu Jenerali James Mattis ametoa ushuhuda katika bunge huko Capitol Hill Alhamisi na kusema kuwa uwiano wa nguvu za kijeshi za kimataifa uliokuwa umewekwa mara baada ya vita vya pili vya dunia unakabiliwa na tishio kubwa kuliko huko nyuma.

“Nafikiri unakabiliwa na hujuma kubwa kuliko zote tangu vita vya pili vya dunia vimalizike na hilo linatokana na Russia, vikundi vya kigaidi na kile ambacho China inafanya katika eneo la South China Sea,” Mattis alisema wakati akijibu swali kwenye mahojiano yake katika hatua za kuthibitishwa mbele ya kamati ya seneti ya huduma za kijeshi.

Mattis amesema “kujihami ni kitu cha dharura hivi sasa” lakini akaongezea kusema kuwa majeshi ya Marekani hivi sasa hayana nguvu za kutosha kukabiliana na changamoto hizi.

Mattis amewaambia wabunge kwamba rais wa Russia, Vladimir Putin “anajaribu kuuvunja umoja wa majeshi ya NATO, “ kampeni inayoilazimu Marekani na washirika wake kuanza kujihami kwa kuunganisha nguvu zao za kidiplomasia, uchumi na kijeshi kujibu hujuma hizo.

Mattis ametoa ushuhuda kuwa yeye na rais mteule wamefanya mazungumzo juu ya umuhimu wa umoja wa NATO ambao ameueleza kama moja ya ushirikiano wa kijeshi wenye mafanikio makubwa “pengine milele.”

Lakini kwa kuwa sheria inawazuia maafisa wa jeshi kuwa mawaziri wa ulinzi mpaka kipite kipindi cha miaka saba baada ya kustaafu kwao, hivyo bunge la Marekani litalazimika kupitisha uteuzi huu ikiwa ni hali ya kipekee kwa mara hii.

Kamati ya huduma za kijeshi imepangwa kulizungumzia suala hili ambalo ni nadra kutokea mara tu baada ya jina la mteule huyu kupitishwa.

XS
SM
MD
LG