Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 06, 2022 Local time: 00:28

Kiir na Machar kukutana ana kwa ana Addis Ababa


Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (R) akizungumza na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry, Juba, Mei 2, 2014.
Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini, Riek Machar amewasili mjini Addis Ababa kwa mazungumzo yake ya kwanza ya moja kwa moja na Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir tangu mapigano na ghasia za kikabili zilipozuka mwezi Disemba mwaka jana.

Machar aliwasili katika mji mkuu wa Ethiopia Alhamis usiku. Rais Kiir anatarajiwa kuwasili, Ijumaa kuanza mazungumzo yanayosimamiwa na kundi la nchi za Afrika mashariki-IGAD. Mashauriano kati ya wajumbe wa waasi na serikali yanaendelea kwa miezi kadhaa kukiwa na mafanikio kidogo.
Riek Machar
Riek Machar


Rais Kiir alikubali kuhudhuria mazungumzo na Makamu Rais wake wa zamani Riek Machar baada ya mkutano na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry nchini Sudan Kusini wiki iliyopita. Muda mfupi baada ya ziara hiyo Marekani ilitangaza vikwazo vyake vya kwanza kuhusiana na mgogoro wa Sudan Kusini.

Vikwazo vili-ilenga serikali na kiongozi mmoja wa waasi waliohusishwa na ghasia ambazo zimesababisha vifo vya maelfu ya watu tangu mapigano yalipozuka kati kati ya mwezi Disemba mwaka jana na kuwakosesha makazi zaidi ya watu milioni moja wengine.
XS
SM
MD
LG