Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 24, 2023 Local time: 16:40

Mkataba wa amani wa Sudan Kusini uko mashakani


Kiongozi wa zamani wa uasi Sudan Kusini, Riek Machar akipeana mkono na Rais Salva Kiir baada ya kutiwa saini kwa mkataba wa amani Agosti 2015.

Wakati Sudan Kusini ikiendelea kujitoa kwenye mzozo, taasisi ya kieneo IGAD, Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa wanajaribu kubuni suluhisho ikiwemo kufikiria pendekezo la kupeleka kikosi kuiongezea nguvu tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo.

Baada ya miezi 20 ya ghasia nchini Sudan Kusini, mkataba wa amani ulitiwa saini Agosti 2015 ambao dhamira yake ni kumaliza mapigano kati ya majeshi hasimu ya rais Salva Kiir na makamu rais wa zamani, Riek Machar wa kundi la SPLM -IO.

Lakini kutokukubaliana kuliendelea na ghasia mpya ziliiubika mji mkuu Juba mwezi Julai, ingawaje sitisho la mapigano linaendelea mjini humo.

Ndani ya mazingira ya ukosefu wa uthabiti, wengi wana hoji iwapo mkataba wa amani una maana yoyote kwa wakati huu.

Kaimu mwakilishi wa SPLM-IO kwa Kenya, Lam Jock anasema majeshi ya Kiir bado yanamlenga Riek Machar, moja ya sababu kuu kwanini mkataba wa amani unalega lega.

Ombi la majibu kutoka kwa msemaji wa kiir halikujibiwa.

Balozi mstaafu wa Sudan na afisa wa Umoja wa Mataifa, Nureldin Satti ameelezea matumaini kuwa Sudan Kusini bado inaweza kujiweka sawa na mkataba wa amani wa Agosti 2015 ukaokolewa.

Lakini Steve Mcdonald wa kituo cha kimataifa cha Woodrow Wilson chenye makao yake Washington DC ana mashaka kuhusu mkataba wa amani wa 2015 kama utarejea katika hali ya kawaida hasa ikizingatiwa kuzuka tena kwa ghasia mwezi Julai mjini Juba, na kuondoka kwa Machar nchini humo.

Anasema inagawaje wahusika wa kimataifa ikiwemo wale wa kieneo IGAD na AU wanajaribu kuweka mambo sawa, kuna matumaini madogo kwamba mkataba wa amani kati ya Machar na Kiir unaweza kufanya kazi.

Satti anasema hali ya usalama lazima iwe thabiti nchini Sudan Kusini kabla ya maendeleo ya kweli kupatikana, na kwa maslahi ya nchi na matararajio ya muda mrefu na kuongeza kuwa Kiir na Machar lazima wamaliza tofauti zao.

Nchi hiyo hivi sasa inasubiri kuona iwapo baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litapitisha azimio ambalo limesambazwa na Marekani kutaka kuidhinishwa kwa kikosi cha wanajeshi 4,000 kwenda Juba.

XS
SM
MD
LG