Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 21:34

Kibaki akata kuidhinisha mswada wa mamlaka ya mikoa


Ndani ya bunge la Kenya wakati wa mjadala wa kikao cha kawaida.
Ndani ya bunge la Kenya wakati wa mjadala wa kikao cha kawaida.

Bunge la Kenya limeanza mvutano mkubwa na afisi ya rais kuhusu mamlaka ya utawala wa mikoa.

Tume ya mageuzi ya sheria Kenya na ile ya utekelezaji wa katiba zimeungana na Rais kwa kueleza kwamba bunge lilifanya makosa lilipoamua kwamba utawala wa majimbo unabidi kuwa chini ya mamlaka ya serikali za mikoa.

Lakini wabunge wamesimama kidete na kutetea msimamo wao wakimtaka rais Mwaki Kibaki maelezo yake ya kumtaka Spika wa bunge Kenneth Marende kufana mabadiliko katika mswada walompelekea.

Misimamo hiyo inayotofautiana huwenda ikachelewesha kutekelezwa sheria muhimu za katiba alisema mbunge wa Budalangi Ababu Namwamba alipozungumza na sauti ya Amerika siku ya Jumanne.

Bw. Namwamba anasema ikiwa mvutano huo utaendelea basi wananchi ndio wataumia zaidi.

Wakati uwamuzi huo wa rais ulipotangzwa, wabunge wa Kenya walikua wamesitisha mjadala bungeni juu ya ripoti kuhusiana na mipaka mipya ya wilaya za uchaguzi kulalamika dhidi ya mageuzi yaliyopendekezwa na kamati ya Mahakama na Sheria.

XS
SM
MD
LG