Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 05:05

Kesi ya Malkia wa Pembe za Ndovu yaahirishwa tena Tanzania


Polisi wa kike akimsindikiza malkia wa pembe za ndovu
Polisi wa kike akimsindikiza malkia wa pembe za ndovu

Kesi ya pembe za ndovu inayomkabili mwanamke raia wa China Yang Feng Glan maarufu kama "Malkia wa Pembe" imeahirishwa tena mjini Dar es salaam, Tanzania.

Hassan Kiangio wakili wa utetezi amesema kuwa amesikitishwa na uamuzi wa mahakama wa kuendelea kufanya uchunguzi zaidi kwa sababu imekuwa ni miaka miwili na nusu sasa tokea kesi hiyo ianze. Wakili huyo ametoa mfano wa kesi nyingine inyofanana na hiyo ambayo ilifanyika mkoani Mbeya na maamuzi kutolewa ndani ya wiki mbili.

Yang Feng Glan "Malkia wa Pembe"
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:59 0:00

Wakili mwingine wa utetezi, Nehemia Nkoko amesema upande wa upelelezi hauna ushahidi wa kupeleka mahakamani na ndio sababu ya kucheleweshwa kwa kesi hiyo.

Faraja Nchimbi ambaye ni wakili mkuu wa serikali amesema maelezo yaliyotolewa na mkurugenzi wa mashtaka ni sahihi na ya kisheria. Amesema mkurugenzi wa mashtaka ana haki ya kisheria kuamua kuendelea na upelelezi zaidi kama anaona kuna ulazima wa kufanya hivyo.

XS
SM
MD
LG