Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:26

Laurent Gbabgo akana mashtaka katika mahakama ya ICC


Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo
Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo

Gbagbo na mshitakiwa mwenzake aliyekuwa kiongozi wa vijana, Charles Ble Goude wanatuhumiwa kula njama za kufanya mashambulizi ya kikatili dhidi ya wafuasi wa kiongozi wa upinzani.

Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo alisema hana hatia Alhamisi katika siku ya kwanza ya kusikilizwa kesi yake katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu huko The Hague.

Gbagbo ni kiongozi wa kwanza wa nchi wa zamani kushitakiwa The Hague anakabiliwa na makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, ikiwa ni pamoja na ubakaji na mauaji kwa kuhusika kwake katika ghasia za baada ya uchaguzi 2010 na 2011 zilizopelekea watu 3000 kufariki dunia.

Waendesha mashitaka wanasema Gbagbo mwenye umri wa miaka 70 na mshitakiwa mwenzake kiongozi wa vijana Charles Ble Goude walikula njama za kufanya mashambulizi ya kikatili dhidi ya wafuasi waliokuwa wakimuunga mkono mpinzani wake Alassane Ouattara baada ya Ouatarra kutangazwa mshindi katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais.

XS
SM
MD
LG