Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 06, 2022 Local time: 20:23

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani kuzuru Kenya


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry anatarajiwa kuwasili nchini Kenya Jumatatu kujadili masuala ya utalii katika nchi jirani kabla ya kwenda Nigeria na Saudi Arabia.

Kerry kwanza atakutana na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kujadili masuala ya kieneo kama vile mgogoro katika nchi jirani ya Sudan Kusini na ghasia zinazoendelea huko Somalia.

Baadae atakwenda Nigeria kukutana na Raisi Muhammadu Buhari katika nchi iliyo na mzozo mbaya wa uchumi na ufisadi pamoja na vitisho vya kundi la wanamgambo wa Boko haram vinavyoendelea.

Kundi la boko haram linalowajibika kwa utekaji wa wasichana 300 kutoka kwenye shule ya Chibok mwaka 2014 , limeuwa takriban watu elfu 20 ndani ya kipindi cha miaka 7 ya uasi wake dhidi ya serikali ya Nigeria.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG