Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, amezitaka pande zinazopingana katika mgogoro wa bahari ya “South China” kumaliza tofauti kwa kuzuia masuala ya kuhodhi ardhi, kijeshi, na ujenzi wa miradi katika eneo hilo.
Bwana Kerry alisema hayo Alhamisi katika mkutano na wanahabari mjini Kuala Lumpur, Malaysia, kuhusu mgogoro unaohusisha mataifa ya kusini mashariki mwa Asia.
Katika majumuisho ya mkutano huo mjadala mkubwa ulihusu mgogoro wa eneo la bahari ya “South China” wakati mataifa ya kusini mashariki mwa Asia yalipojaribu kutoa kauli moja ya kumaliza mgogoro.
Utata wa ujenzi wa miradi ya China katika bahari ya “South Sea,” ambapo baadhi ya majirani zake wamekuwa wakipinga hatua hiyo, ulikuwa ni ajenda muhimu ya mkutano wa Kuala Lumpur.