Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 13:05

Kerry asema Marekani na wadau wake wanuia kumaliza ghasia Syria


Waziri wa mambo ya anje wa Marekani John Kerry katika picha
Waziri wa mambo ya anje wa Marekani John Kerry katika picha

Waziri huyo wa Marekani hakuweka bayana mapendekezo halisi lakini amekuwa akitaka kurejesha makubaliano ya amani na kusitisha mashambulizi ya vikosi vya serikali ya Syria.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry amemaliza ziara yake iliyochukuwa saa 20 mjini Geneva Jumatatu na kusema Marekani na washirika wake wanajadili mapendekezo kadhaa ya kumaliza ghasia za Syria.

Mwanadiplomasia huyo wa Marekani hakuweka wazi juu ya mapendekezo halisi, lakini malengo yake yamekuwa ni kurudisha sehemu ya makubaliano ya amani na kusitisha mashambulizi ya vikosi vya serikali ya Syria yanayoungwa mkono na Russia, ambayo yamesababisha vifo vya mamia ya watu mjini Aleppo katika siku 11 zilizopita.

Mashirika ya habari yamenukuu maafisa wa Marekani ambao hawakutaka kutajwa majina wakisema Marekani inataka kutenga eneo ambalo litakuwa salama kwa wakimbizi na wanachama wa upinzani wa kati.

XS
SM
MD
LG