Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 22, 2024 Local time: 10:15

Kerry anakutana na viongozi wa Ubelgiji na EU


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry (L) na Waziri Mkuu wa Ubelgiji, Charles Michel wakiwa Brussels, March 25, 2016.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry (L) na Waziri Mkuu wa Ubelgiji, Charles Michel wakiwa Brussels, March 25, 2016.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry anafanya mkutano na viongozi wa Ubelgiji na Umoja wa ulaya mjini Brussels akitoa salamu za rambi rambi za Marekani kwa watu wote ambao walipoteza maisha yao au walijeruhiwa katika shambulizi lililotokea Jumanne mjini Brussels.

Ofisa mmoja mwandamizi wa Marekani alithibitisha kwamba raia wawili wa Marekani walikuwa miongoni mwa zaidi ya watu 30 waliouwawa kwenye shambulizi hilo. Waziri Kerry hakutoa maelezo zaidi juu ya raia hao zaidi ya kusema kwamba mmoja kati ya raia hao waliokufa alikuwa mtoaji mafunzo ambaye alikuwa akirudi Marekani kwa ajili ya sherehe za sikukuu ya Pasaka.

Bwana Kerry alisema Marekani na wanachama wa ushirika wana ujumbe kwa kila mtu ambaye ataua na kuwajeruhi raia wasio na hatia na kukatisha maisha yao ya kila siku. “Kamwe hatutatishika”.

Bwana Kerry alikutana na Waziri Mkuu wa Ubelgiji, Charles Michel kwenye makazi ya Waziri Mkuu. Bwana Michel alimshukuru Kerry kwa kuwepo huko na aliapa kufanya kazi kadri awezavyo na Marekani na marafiki zake wa ulaya ili kuzuia mashambulizi yeyote ya baadae.

XS
SM
MD
LG