Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 14:25

Kerry anaitembelea miji ya Brussels na London


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, anatembelea miji ya Brussels na London siku ya Jumatatu, safari ambayo itakuwa ya kwanza kwa ofisa huyo wa ngazi ya juu wa serikali ya Marekani katika miji hiyo miwili tangu Uingereza ilipopiga kura ya kujitenga na Umoja wa Ulaya wiki iliyopita hatua ambayo imeleta wasiwasi mwingi kwa Washington.

Maafisa wa Marekani walisema kuwa Kerry ambaye ameongeza miji hiyo miwili kwenye ratiba yake ya safari ambayo awali ilikuwa impeleke mjini Rome ataelezea uungaji mkono wa Marekani kwa Uingereza na kusisitiza umuhimu wa mataifa mengine wanachama wa Umoja wa Ulaya kuendelea kuwepo kwenye muungano huo.

Kerry alisema Jumapili kwamba Marekani inasikitishwa na kura hiyo ya Uingereza kuondoka kwenye Umoja wa Ulaya lakini akaapa kuendelea na uhusiano wa karibu na umoja huo ambao utakuwa na mataifa 27 wanachama.

XS
SM
MD
LG