Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 29, 2022 Local time: 01:20

Kerry Apeleka Ahueni Yemen


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, akiongea katika mkutano nchini Djibouti.

Waziri wa mambo ya nje Marekani, John Kerry, amesema mazungumzo kuhusu “kusisitisha mapigano kwa sababu za kibinadamu” Yemen, yatakuwa shauri la msingi na mkutano wake ujao na maafisa wa Saudi Arabia.

Kerry amesema atajadili hali halisi ya msaada huo na namna utakavyoweza kutekelezwa wakati atakapo wasili mjini Riyadh Jumatano jioni.

Alizungumza kutokea Djibout, Jumatano, ambapo alifanya mkutano na Rais Ismail Omar Guelleh, na maafisa wengine. Kerry amesema hali tete ya Somalia, na Yemen, ilikuwa miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa.

Djibout, imechukuwa nafasi muhimu kuwakaribisha Wamarekani, na wageni wengine waliokimbia machafuko ya Yemen, ambapo muungano wa mashambulizi ya anga yanayoongozwa na Saudi Arabia, yamekuwa yakifanyika dhidi ya waasi wa Houthi ambao wameshikilia baadhi ya sehemu za nchi.

Kerry amesema kuna viashirio kutoka pande zilizo katika mgogoro wa Yemen, kuwa tayari kukubali msaada wa kibinadamu.

“Katika mzungumzo yangu ya jana na mawaziri wengine wa mambo ya nje kutoka nchi nyingine, kulikuwa na ishara kwamba, wa Houthi, wanaweza kuwa tayari kukubali msaada huo.” Alisema.

Kerry aliongea hayo katika mkutano wa pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Djibout, Waziri Mohamoud Ali Youssouf.

Msaada wa Marekani kwa Yemen

Katika mkutano huo, pia alitangaza Marekani itatoa msaada mwingine wa kibinadamu wa dola milioni 68 kwa Yemen. Fedha hizo zitatumika kwa upatikanaji wa chakula, maji, malazi, huduma za afya, na misaada mingine.

“Mamilioni ya watu wapo katika mahitaji ya msaada,” alisema waziri Kerry.

Wizara ya mambo ya nje imesema fedha zitasaidia mashirika ya misaada, ambayo yamekuwa yakikabiliana na upungufu wa mahitaji ya watu milioni 16 wa Yemen walioathirika na mgogoro wa unaoendelea, ikijumuisha wale 300,000 ambao wamekosa makazi nchini humo.

Kabla ya ziara ya Kerry, nchini Djibouti, afisa wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje, amesema zaidi ya raia wa Marekani 500 waliondoka Yemen walipitia Djibouti, pamoja na idadi sawa ya familia zao. Maafisa wamesema idadi ya raia wan je wanaoondoka Yemen imekuwa ipo pale pale.

Pamoja na kukutana na rais wa Djibouti, na waziri mkuu, Kerry alitembelea msikiti, ambapo aliongea na vijana, ikijumuisha wale walioshiriki walioshiriki mkutano ulioandaliwa na Marekani wa viongozi vijana wa Afrika YALE.

Pia alikutana na wanajeshi wa Marekani katika kambi ya Lemonnier. Kambi hiyo ya Marekani ina wafanyakazi karibu 4,500, wanaohudumia juhudi za kijeshi za Marekani katika eneo la pembe ya Afrika.

Kerry alisafiri kwenda Djibouti, akitokea Kenya, ambapo alikutana na viongozi wa kisiasa, na wale wa asasi za kiraia. Vilevile alifanya ziara iliyokuwa si rasmi nchini Somalia, Jumanne, na kuwa kuwa waziri wa mambo ya nje wa kwanza kutoka Marekani kutwmbwlw nchi hiyo akiwa madarakani.

Baadaye, Kerry alikamilisha ziara yake kwa kuelekea Saudi Arabia, amesafiri kwenda Paris, Ufaransa ambapo atakutana na wanachama wa baraza muungano la Uajemi kujadili usalama, na ushirikiano wa kikanda.

XS
SM
MD
LG