Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:22

Serikali ya Kenya yagawa Laptop kwa wanafunzi wa shule za msingi


Wanafunzi wakiwa darasani kwenye shule ya Youth for Technology Foundation mjini Nairobi.
Wanafunzi wakiwa darasani kwenye shule ya Youth for Technology Foundation mjini Nairobi.

Katika kile kinachoonekana kama jitihada za kutimiza na kutekeleza ahadi zake kabla ya uchaguzi mkuu mwaka ujao, Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, imetangaza rasmi kuanza kuwapa wanafunzi wote wa shule za msingi za umma nchini humo vipakatalishi, yaani laptop kuanzia Ijumaa Septemba 30 na litakamilika katika kipindi cha mwezi mmoja.

Mara tu baada ya kuchaguliwa mwaka 2013, Rais Kenyatta aliahidi kuyafanya masomo kuwa kwenye mfumo wa kidigitali kwa kuwapa wanafunzi wote wa shule za umma nchini humo vipakatalishi hivyo.

Likiwa ni zoezi lililotarajiwa kwa hamu kubwa kote nchini, serikali hatimaye imeanza mchakato wa kuwapa wanafunzi wa shule za msingi za umma vipakatalishi vitakavyowawezesha kufuatilia masomo katika mfumo wa kidigitali. Japo zoezi hili halijafika wakati alioutangaza Rais, serikali yake imekuwa mbioni kuhakikisha kuwa ahadi muhimu alizozitoa mara tu baada ya kuchaguliwa kwake zinatimizwa.

Waziri wa Elimu nchini humo, Fred Matiang’i anasema kuwa vipakatalishi hivyo vimeundwa kwa mtaala wa kisasa na hivyo basi utawawezesha wanafunzi na shule za umma kuukumbatia mfumo wa kidigitali unaokumbatiwa na mataifa yaliyoendelea. Bwana Matiang’i akiahidi kutoa tangazo la kuidhinishwa kwa mtaala mpya wa mafunzo kwa walimu kote nchini.

Naye waziri wa Sayansi na Teknolojia, Joe Mucheru aanasema kuwa serikali tayari imewapa mafunzo ya kutosha walimu watakaobeba jukumu la kuwaongoza wanafunzi kote nchini kupata mafunzo muhimu jinsi ilivyo katika mtaala.

Suala ambalo limeonekana kuwa tete ni iwapo shule za msingi za umma takriban milioni moja nukta mbili zimejengewa miundo msingi inayofaa kama vile umeme. Waziri wa Kawi Charles Keter anaeleza kuwa shule zote zitakuwa na umeme kabla ya mwaka huu kumalizika.

Zaidi ya vipakatalishi 1,060 tayari vimepokelewa nchini na nyingine zipatao 22,000 zikitarajiwa kufika nchini kila wiki.

XS
SM
MD
LG