Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 21, 2023 Local time: 07:18

Kenyatta na Desalegn wako Juba kwa mazungumzo na rais Kiir


Waziri Mkuu wa Ethiopia, rais Salva Kiir wa Sudan (katikati) na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (kulia) mjini Juba Dec.26,2013
Juhudi za viongozi wa kikanda zinazolengaa kufikia maelewano ya amani katika mgogoro wa Sudan Kusini zinaendelea, huku viongozi wa Kenya na Ethiopia wakiwa Juba kwa mazungumzo.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn wanakutana na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir leo Alhamis katika mji mkuu wa Juba.

Bw. Kiir anamshtumu makamu rais wake wa zamani Riek Machar kwa kupanga njama za jaribio la kupindua serikali yake,swala lililozusha mapigano makali nchini humo yapata siku 11 zilizopita.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanakisia kuwa maelfu ya watu wameuawa katika ghasia hizo ambazo zinawahusisha zaidi watu wa makabila mawili, lile la Kiir la Dinka na lile la Machar la Nuer.

Machar ambaye ametoroka na hajulikani aliko amekanusha kujaribu kupindua serikali , lakini amesema jeshi la Sudan Kusini linapaswa kumwondoa madarakani bwana Kiir. Zaidi ya watu elfu 40 wametafuta hifadhi katika vituo vya Umoja wa Mataifa kutokana na mapigano yanayoendelea nchini humo.

Mapigano ya hivi karibuni yamo katika mji wa Malakal, mji mkuu wa jimbo la Upper Nile lenye utajiri wa mafuta,kati ya waasi na majeshi yanayounga mkono serikali.Mapema wiki hii serikali ilikomboa mji muhimu wa Bor ulioko jimbo la Jonglei kutoka kwa wapiganaji waasi.
XS
SM
MD
LG