Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 19:58

Rais Kenyatta avunja safari ya nje kufuatia shambulizi Mandera


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amevunja safari ya kwelekea Angola, baada ya shambulizi la kigaidi kuuwa watu 12 mjini Mandera, Kenya.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amevunja safari ya kwelekea Angola, baada ya shambulizi la kigaidi kuuwa watu 12 mjini Mandera, Kenya.

Kufuatia shambulio lililotokea mapema leo katika mji wa Mandera nchini Kenya na kuwaua watu kumi na wawili na kuwajeruhi wengine, rais Uhuru Kenyatta amevunja ziara aliyokuwa amepanga kufanya nchini Angola, na badala yake akamtuma naibu wake, William Ruto kumwakilisha.

Taarifa iliyotolewa na ikulu ya Nairobi ilisema kuwa rais huyo amechukua hatua hiyo ili kulishughulikia swala hilo la shambulizi.

Mapema leo, maafisa wa Kenya walisema kuwa shambulizi lililowalenga watu wasio wa dini ya kiislamu kwenye mpaka wa kaskazini mashariki na Somalia liliwauwa watu 12. Kamanda wa polisi katika kaunti ya Mandera Job Boronjo amesema kuwa wanamgambo wanaoaminika kutoka kundi la al-Shabab lenye makao yake Somalia wameshambulia kwa maguruneti na vilipuzi vya kujitengenezea, jengo lenye vyuma vya kulala wageni la Bisharo ambalo kwa kawaida hutumiwa na watu wa kutoka mbali na eneo hilo. Kundi al Shabab muda mfupi baadaye kupitia mtandao wake wa Telegram, lilidai kuhusika likisema kuwa lililenga wafanyakazi wa kikristo. Shambulizi hilo ni mojawapo ya mengine mengi yaliotekelezwa na kundi hilo karibu na mpaka huo tangu Kenya ilipopeleka majeshi yake nchini Somalia mwaka wa 2011. Mapema mwezi huu, watu 6 waliuwawa mjini Mandera kwenye shambulizi sawa na hilo.

XS
SM
MD
LG