Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 24, 2020 Local time: 15:28

Kenyatta atia saini sheria ya kudhibiti riba ya benki Kenya


Rais Uhuru Kenyatta atia saini mswada wa kudhibiti viwango vya riba nchini. Jumatano Agosti 24, 2016

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, siku ya Jumatano alitia saini na kuufanya sheria mswada uliowasilishwa kwake na bunge kuhusu viwango vya riba vinavyotozwa na benki nchini humo.

Sasa viwango vya riba inayotoizwa na benki havitapita asili mia nne na vitaendelea kudhibitiwa na serikali.

Benki kuu ya Kenya inatoza asili mia 10.5 kwa sasa. Hii ina maana kuwa mtu anyepewa mkopo na benki nchini Kenya, hafai kulipa zaidi ya asili mia 14.5 kwa riba.

Aidha, mtu anayeweka pesa zake hawezi kutarajia zaidi ya asili mia 14.5 ya riba kutoka kwa benki.

Mswada huo ulipitishwa na bunge mwezi wa Julai na ulikuwa unasubiri saini ya rais.

Kumekuwa na vuta nikuvute kati ya wamiliki wa benki na wateja, huku benki zikishikilia kwamba kudhibiti viwango zinavyotoza wateja wake kutaathiri uchumi wa nchi na uwekezaji.

Facebook Forum

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG