Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 05:08

Kenyatta aomba radhi kwa taifa


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameomba radhi kwa taifa kutokana na madhambi yaliyopita ambayo yalifanywa na serikali yake na zile zilizopita nchini humo.

Akihutubia bunge katika hotuba ya hali ya taifa Alhamisi Rais Kenyatta alisema wakati umefika kufunga ukurasa wa machungu ya zamani. Rais Kenyatta alitaja mauaji ya ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007/8 na mauaji ya maelfu ya raia wa Kenya wenye asili ya Somalia kama baadhi ya madhambi ya kihistoria katika nchi hiyo.

Mwezi Disemba 2014 waendesha mashitaka katika mahakama ya jinai ya kimataifa (ICC) huko The Hague walifuta mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu yaliyokuwa yanamkabili Bw. Kenyatta kufuatia kile kilichodaiwa ni kuhusika kwake katika ghasia za baada ya uchaguzi.

Ripoti ya Tume ya Maridhiano ya Ukweli na Haki ya Kenya ilipendekeza mwaka 2013 rais Kenyatta aombe radhi kwa umma. Ripoti hiyo ilimtaja rais na makamu wake William Ruto kuwa miongoni mwa wale wanaoshukiwa kupanga na kufadhili ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007/8.

Serikali za Kenya zilizopita - hasa za marais Jomo Kenyatta (baba yake Uhuru Kenyatta) ambaye aliongoza Kenya kutoka uhuru wa nchi hiyo mwaka 1964 hadi alipofariki mwaka 1978, na rais Daniel arap Moi kutoka 1978 mpaka 2002 mara nyingi zimeshutumiwa kwa vitendo vibaya dhidi ya baadhi ya raia wa nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG