Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 03:01

Kenyatta aahidi uchunguzi wa kina kufuatia shambulizi la polisi


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ameahidi kwamba serikali yake itafanya uchunguzi wa kina ili kujua kiini cha mkasa uliopelekea kuuawa kwa maafisa saba wa polisi na polisi mwenzao kaskazini magharibi mwa kenya siku ya Alhamisi.

Katika taarifa iliyotolewa na ikulu ya Nairobi, Kenyatta alitoa rambirambi kwa jamaa wa maafisa waliouawa na kusema mpaka sasa haijabainika kile kilichopelekea shambulizi hilo. Aidha Kenyatta aliahidi msaada kwa familia za waathiriwa.

Kufuatia makabiliano makali, Maafisa wa kikosi maalumu cha Recce walimuua polisi muasi aliyeua wenzake saba na kuteka nyara kituo hicho cha polisi kilicho katika kaunti ya Pokot Magharibi kwa muda wa saa nane. Taarifa za awali kutoka kwa mkuu wa polisi nchini humo zilisema kuwa mtu aliyetekeleza shambulizi hilo huenda alikuwa na uhusiano na kundi la wanamgambo la Al-Shabaab lenye makao yake kutoka Somalia.

XS
SM
MD
LG