Na BMJ Muriithi
Waziri wa Usalama wa ndani nchini Kenya Joseph Nkaissery, siku ya Jumanne alikanusha ripoti iliyochapishwa na gazeti moja nchini humo - Daily Nation - mnamo mwishoni mwa wiki, iliyowashutumu maafisa wa polisi kwa kile ilichokiita mauaji ya kiholela ya wananchi. Akizungumza na Sauti ya Amerika kwa njia ya simu, Nkaissery alianza kwa kueleza hisia zake kuhusu ripoti kwamba zaidi ya watu mia mbili wameuawa katika kipindi cha mwaka mmoja.