Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 19, 2025 Local time: 02:57

Kenya yatia saini mkataba wa kihistoria wa kibiashara na EU


Rais wa Kenya William Ruto na mkuu wa EU Ursula von der Leyen mjini Nairobi Jumatatu.
Rais wa Kenya William Ruto na mkuu wa EU Ursula von der Leyen mjini Nairobi Jumatatu.

Kenya na Umoja wa Ulaya Jumatatu wametia saini  makubaliano yatakayotoa  nafasi kwa taifa hilo la Afrika Mashariki kupeleka bidhaa zake bila kulipa ushuru, pamoja na kuingia kwenye mataifa ya Umoja huo bila masharati, maafisa wa serikali wamesema.

Mkataba huo ndiyo mkubwa zaidi wa kibiashara kati ya EU na taifa la kiafrika tangu 2016. Wakati wa hafla hiyo iliyohudhuriwa na mkuu wa EU Ursula von der Leyen, rais wa Kenya William Ruto amesema kwamba lengo kubwa la mkataba huo ni kuhakikisha wakenya wanaweka pesa kwenye mifuko yao.

Von der Leyen kwa upande wake amesema kwamba huo ni ushindi kwa kila upande, wakati akiomba mataifa mengine ya kiafrika kujiunga, ukifuatia miaka kadhaa ya mashauriano yaliokamilika Juni.

Waziri wa biashara wa Kenya Rebecca Miano amesema kwamba “ Makubaliano ya leo yanafungua ukurasa mpya kwa bidhaa za Kenya kuingia kwenye soko la EU bila kulipa ushuru”,wakati wa hafla hiyo iliyofanyikia mjini Nairobi.

Kenya huuza majani chai, kahawa, maua, matunda pamoja na mboga kwenye soko la EU, ikiwa ni asilimia 21 ya jumla ya mauzo yake kwenye masoko ya nje. Tiafa hilo pia huagiza mashine, dawa pamoja na kemikali kutoka mataifa la EU.

Forum

XS
SM
MD
LG